Wasyria walioko uhamishoni wahofia kusakwa na serikali
5 Aprili 2018Wasyria wanaoishi katika nchi zengine kwa sasa wanatumia muda mwingi mtandaoni wakiandika majina yao kuanzia jina la kwanza la kati na jina la ubini, ili kutafuta orodha ya majina yaliyopo mtandaoni.
Wengi wana wasiwasi kuwa kufika tena Damascuss mji mkuu wa Syiria, kutawaweka katika magereza ya serikali au katika hali mbaya zaidi.
Maelfu ya raia wamekamatwa na vyombo vya usalama vya Syria tangu mgogoro ulipotokea mwaka 2011, wengi wakiwa wanaipinga serikali iliyopo madarakani.
Wengi wameikimbia nchi yao kwa kuogopa kuwekwa kizuizini, kupata mateso au hali nyingine mbaya zaidi. Tovuti ya Zaman Al-Wasl inayomilikiwa na wafuasi wa upinzani ilichapisha orodha ya utafiti ya watu milioni 1.5 wanaotafutwa ikiwamo idara la usalama.
Tovuti ya Zaman Al-Wasl iliandika kuwa orodha hiyo ya watu wanaotafutwa ni sehemu ya orodha nyingine ya watu milioni 1.7 majina yaliyovuja kutoka katika nyaraka za serikali. Inaonesha kuwa orodha ya majina hayo mtandaoni imetafutwa zaidi ya mara 10.
Tovuti hiyo pia inaonesha jinsi watu walivyopatwa na mshangao na wasiwasi baada ya kubaini kuwa wanatafutwa. Wakati majina 500,00 ya awamu ya kwanza yalipotolewa mwanzoni mwa mwezi Machi, wafuasi wa upinzani Syria walianza kutumiana habari hiyo kwenye mitandao.
Orodha hiyo haioneshi hasa wazi kuhusu uhalifu na wasi wasi unabaki kuwa ni orodha mpya au iliyopitwa na wakati. Wakati Zeina Raina wa Syria alipogundua kuhusu orodha hiyo moyo wake ulipata wasiwasi. Aliondoka Syria mwaka 2012 baada ya kutumikia kifungo gerezani kwa miaka miwili na sasa anajiuliza kama atakutana na kifungo tena kwa mara ya tatu.
Zeina anaifananisha hali hiyo ya orodha ya majina ya watu wanaotafutwa kama kusubiri vipimo vya ugonjwa ambao unajua unao lakini bado unasubiri vipimo.
Dibrin Mohammad mwenye umri wa miaka 37 anayeishi eneo linalodhibitiwa na Wakurdi la Qamishli anasema kuwa hata watu wanaoishi nje ya utawala wa Syria wanaitumia tovuti ya Zaman-al-Wasl's, lakini wakati huo huo anahofia kukamatwa kwa kosa la kuipinga serikali mwaka 2011.
Mwandishi: Veronica Natalis /AFP
Mhariri: Iddi Ssessanga