BiasharaSudan Kusini
UN: Sudan Kusini kupata mkopo wa dola bilioni 13 kutoka UAE
18 Mei 2024Matangazo
Hayo yanaarifiwa licha ya matatizo ya nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta kushindwa kudhibiti madeni yatokanayo na akiba yake ya mafuta.
Jopo hilo la wataalamu limesema katika ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba hati za mkopo ilizopata nakala yake, zinaonyesha makubaliano kati ya Sudan Kusini na kampuni ya Hamad Bin Khalifa, na ambao utakuwa mkopo mkubwa zaidi kuwahi kutolewa.
Ujumbe wa UAE katika Umoja wa Mataifa haukuzungumzia chochote kuhusu makubaliano hayo na kusisitiza kuwa kampuni hiyo ni ya watu binafsi. Kulingana na mamlaka ya Marekani inayohusika na masuala ya nishati, Sudan Kusini ilizalisha mwaka jana wastani wa mapipa 149,000 ya mafuta.