1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wataalamu: Olimpiki isitishe ushirikiano na Coca-Cola

7 Agosti 2024

Wataalamu wawili wa masuala ya afya wamewataka waandaaji wa mashindano ya Olimpiki wavunje uhusiano na kampuni ya Coca Cola.

Michezo ya Olimpiki inaendelea mjini Paris, Ufaransa
Michezo ya Olimpiki inaendelea mjini Paris, Ufaransa. Picha: Matthias Schrader/AP/picture alliance

Wataalamu hao wameeleza kuwa fedha nyingi za ufadhili zinaiwezesha kampuni hiyo ya Marekani kueneza vinywaji vyenye sukari nyingi visivyokuwa vya afya.

Mabingwa hao wa afya wameandika kwenye jarida la afya la Global Health, kutanabahisha zaidi kwamba bidhaa za kampuni ya Coca Cola pia zinachangia katika kuhatarisha mazingira kutokana na gesi chafu na matumizi ya maji ya kiwango kikubwa.

Wanasayansi hao wawili wameiambia kamati ya kimataifa ya Olimpiki kwamba, kwa kuendeleza uhusiano na kampuni ya Cocacola kamati hiyo pia inajitia hatiani katika uharibifu wa mazingira.