UN: Rwanda inatoa ameri kwa waasi wa M23 Mashariki mwa Kongo
2 Julai 2025
Operesheni hizo ziliwapa waasi hao ushawishi wa kisiasa na kufikia eneo lililo tajiri kwa madini nchini humo.
Ripoti hiyo iliyoonekana na shirika la habari la reuters, imesema Rwanda imetoa mafunzo kwa kundi hilo, vifaa vya kijeshi vinavyojumuisha mifumo ya teknolojia ya hali ya juu inayoweza kupambana na jeshi la Kongo.
Kundi hilo la M23 limepiga hatua katika vita vyake Mashariki mwa Kongo na mwezi Januari na Februari lilifanikiwa kudhibiti miji miwili muhimu ya Goma na Bukavu.
Mahakama ya Afrika ya Haki inayo mamlaka ya kusikiliza kesi ya DRC vs Rwanda
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Marekani na Mataifa ya Magharibi, wanaamini Rwanda inawaunga mkono waasi hao wa M23 kwa kuwapa silaha na wanajeshi wanaowasaidia kupambana na jeshi la FARDC
Rwanda hata hivyo imeendelea kukanusha madai hayo ikisema wanajeshi wake wamechukua hatua, ili kujilinda dhidi ya jeshi la Kongo na wanamgambo wa kihutu wa FDLR wanaofungamanishwa na mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka 1994.