Sheria na HakiAfrika
Wataalamu wa UN waelezea ukiukwaji wa haki Zambia
30 Agosti 2024Matangazo
Wataalamu watatu wa Umoja wa Mataifa walisema hapo jana kwamba kumekuwa na tuhuma nyingi za kuwekwa kizuizini kwa madai yanayohusiana na mikusanyiko isiyo halali pamoja na madai ya ujasusi, matamshi ya chuki na vitendo vya uchochezi.
Walengwa katika madai hayo ni viongozi wa vyama vya upinzani na wanachama, wabunge na watetezi wa haki za binadamu, huku marufuku ikiwekwa dhidi ya mikutano na maandamano ya amani.
Soma pia:Ethiopia imeshindwa kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu
Mapema mwezi huu, kiongozi wa chama kidogo cha upinzani nchini humo, Fred M'membe, alikamatwa kuhusiana na chapisho lake la kwenye mitandao ya kijamii huku polisi wakilitaja kuwa kosa la vitendo vya uchochezi.