1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Ujerumani yafanya juhudi kuondoa ukomo wa kukopa

Angela Mdungu
5 Desemba 2023

Bunge la Ujerumani leo linawahoji wataalamu kuhusu mipango ya serikali ya kutaka kuondoa ukomo wa kukopa ulioainishwa kikatiba ili kupata fedha za ziada kwa ajili ya bajeti ya mwaka 2024.

Kikao cha bunge la Ujerumani kcha Novemba 9, 2023
Bunge la UjerumaniPicha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Serikali ya mesto ya Kansela Olaf Scholz inayoundwa na muungano wa vyama vitatu inapambana kutafuta namna ya kuondokana na mgogoro wa bajeti ulioibuka mwezi uliopita.

Mgogoro huo ulianza baada mahakama ya katiba kusitisha hatua ya serikali ya Ujerumani kutaka kutumia fedha zilizobakia wakati wa janga la Uviko-19 kwa ajili ya miradi ya hali ya hewa na ruzuku kwa ajili ya nishati.

Uamuzi huo uliipa ushindi kambi ya Upinzani ya vyama vya kihafidhina vya CDU/CSU ambavyo vilipinga hatua ya serikali ya kubadilisha matumizi ya fedha yaliyopitishwa kwenye bajeti.

Soma zaidi: Je, ukomo wa deni la Ujerumani ni nini hasa?

Ikiwa kizingiti hicho cha kisheria cha kuondoa ukomo wa kukopa kitaondolewa, serikali ya Ujerumani itaweza kuidhinisha  dola bilioni 45 ambazo zimepungua.

Kulingana na taarifa ya maandishi, wengi wa wataalamu wanauona mpango wa serikali wa kuondokana na mkwamo huo kuwa unaofaa. Wameandika kuwa Ujerumani ilikuwa katika hali ya dharura mwanzoni mwa mwaka kutokana na tatizo la umeme lililotokana na uvamizi w Urusi nchini Ukraine.

Kulingana na katiba, ukomo wa wezo wa kukopa unaweza kuwekwa kando iwapo kuna dharua ya kitaifa au janga la asili.

Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Kansela Scholz, kutoka chama cha SPD amekuwa na mazungumzo ya kina na Waziri wa uchumi Robert Habeck wa chama cha kijani pamoja na Waziri wa fedha Christian Lindner wa chama cha FDP.

Mgogoro wa bajeti hautazuia Ujerumani kuisaidia Ukraine

Kwa upande wake Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock amesisitiza kuwa mgogoro wa bajeti wa Ujerumani hautoathiri uungaji mkono wa nchi hiyo kwa Ukraine, ingawa hajaweka wazi ikiwa mkutano wa mawaziri untakaofanyika Jumatano utakuwa na makubaliano katika masuala muhimu kwenye bajeti hiyo ya mwaka 2024. Baerbock ameyasema hayo leo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari mjini Lubljana katika ziara yake nchini Slovenia 

Soma zaidi: Bunge la Ujerumani laidhinisha bajeti kubwa kwa jeshi

Mgogoro wa bajeti nchini Ujerumani umefukuta zaidi kati ya vyama vinavyounda serikali, huku vipaumbele vya kila chama kwenye bajeti hiyo vikiwa katika shinikizo kubwa. Chochote kitakachoamuliwa, iwe kupunguza matumizi katika shughuli za kijamii yanayoongezeka, kupunguza fedha katika miradi ya mazingira, ruzuku au kuongeza kodi, kunaweza kuathiri vipaumbele muhimu vya vyama vinavyounda serikali ya pamoja.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW