1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaUganda

Wataalamu wasema mripuko wa Ebola nchini Uganda unadhibitiwa

5 Januari 2023

Shirika la kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika limesema kwamba mripuko wa Ebola nchini Uganda unaelekea kudhibitiwa na siku 39 zimepita tangu kuripotiwa kwa kisa cha mwisho kilichothibitishwa cha virusi hivyo.

Uganda | Ebola Ausbruch
Picha: Luke Dray/Getty Images

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa barani Africa Ahmed Ogwell Ouma, amesema iwapo hakutakuwa na kisa kipya kilizchoripotiwa nchini Uganda kufikia Januari 10 basi mlipuko huo utakuwa umekwisha.

Ouma aliwaambia wanahabari kuwa kufikia sasa kumekuwa na vifo 142  vya Ebola vilivyothibitishwa na vifo 55 katika mlipuko wa Uganda. Majaribio ya chanjo dhidi ya aina ya Ebola ya Sudan yalikuwa yakiendelea.

Aliisifu serikali ya Uganda kwa kuchukua hatua za kuzuia kusambaa kwa Ebola, akisema ilichukua takriban siku 70 za kudhibiti maambukizo hayo huku kukiwa na wagonjwa 142 wakati watu 55 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Ouma ameeleza kuwa, majaribio ya aina ya kirusi cha Ebola kwa jina Sudan, yanaendelea.