1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watafiti Kenya watafuta njia ya kukabiliana na nzige

Josephat Charo
2 Julai 2020

Wakati Afrika Mashariki ikihofia kukabiliwa na wimbi la pili la nzige, watafiti mjini Nairobi nchini Kenya wameanza kufanya utafiti kuhusu njia kadhaa za kuwauwa wadudu hao hatari.

Heuschreckenangriff in den Wohngebieten von Jaipur, Rajasthan
Picha: picture-alliance/NurPhoto/V. Bhatnagar

Kulingana na benki ya dunia, mnamo mwaka huu, huenda wadudu hao wakasababisha eneo la Afrika Mashariki pamoja na Yemen kupoteza kiasi cha pesa chenye thamani ya dola bilioni 8.5 za Marekani.

Kwa kawaida njia ya kuuwa nzige ni kunyunyuzia dawa nzige wadogo ambao bado hawajaanza kuruka. Hata hivyo dawa hiyo imetajwa kuwa na madhara makubwa kwa wadudu wengine pamoja na mazingira.

Watafiti katika kituo cha kimataifa kinachohusika na utafiti wa wadudu pamoja na uhusiano wa viumbe na mazingira (ICIPE), wameanza kuifanyia jaribio dawa yenye uwezo wa kuwauwa nzige ambayo pia ni rafiki kwa mazingira.

Wakati huo huo, wanafanya utafiti kuhusu jinsi ya kuwageuza nzige kuwa chakula kwa binadamu au kwa wanyama kama mojawapo ya njia ya kutokomeza wadudu hao kabisa.

Watafiti wa kituo hicho cha ICIPE, ni miongoni mwa kundi la watafiti waliogundua kuvu aina ya "Metharizium acridum,” kuvu iliyo na uwezo wa kuuwa nzige bila kuwa na athari hasi kwa viumbe wengine.

Kwa sasa, "Metharizium acridum” inatumiwa kuuwa nzige katika eneo la Afrika Mashariki. Mtafiti Baldwyn Torto, alisema utafiti wake umejikita hasa katika kuchunguza harufu ya nzige. Torto alisema nzige ambao bado hawajaanza kuruka wana njia pekee ya mawasiliano kwa kutumia harufu ambayo inawawezesha kubakia katika makundi. Mtafiti huyo anaeleza kuwa harufu hiyo inabadilika pindi nzige hao wanapokomaa.

Watafiti wanaeleza ikiwa harufu hiyo inanyunyiziwa kwa nzige waliokomaa, inaweza kutenganisha makundi yao, kusababisha wadudu hao kulana wao kwa wao na hivyo basi kurahihisha kuuliwa na dawa kwa urahisi.

Chanzo: Reuters

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW