Watafiti: Baadhi ya programu za akili mnemba (AI) ni hatari
29 Juni 2025
Matangazo
Hayo ni baada ya kubainika kuwa baadhi ya programu hizo zenye ufanisi za (AI) ili kufikia malengo yake zinaweza kudanganya, kubuni njama na hata kutoa vitisho.
Katika mfano mmoja wa kutatanisha, mtumiaji mmoja alitishia kuizima programu ya AI inayofahamika kama "Anthropic Claude 4", na ndipo programu hiyo ikamtishia kufichua mahusiano yake ya nje ya ndoa.
Matukio kama haya yanatia wasiwasi baada ya programu ya akili mnemba ya ChatGPT kutikisa ulimwengu karibu miaka miwili iliyopita, lakini yanabainisha ukweli kwamba hata watafiti wa AI bado hawaelewi kikamilifu jinsi ubunifu wao wenyewe unavyofanya kazi.