Wataliban wahujumu kituo cha polisi Afghanistan
23 Novemba 2007Matangazo
Wanamgambo wa Taliban mapema leo asubuhi, wamehujumu kituo cha polisi,kusini mwa Afghanistan na kuwaua askari polisi 7 na wengine 6 wametekwa nyara.Kamanda wa polisi Abdul Hakim Jan amesema,wanamgambo hao waliwazidi nguvu askari polisi 13 katika shambulizo lililotokea katika wilaya ya machafuko ya Kandahar.
Msemaji mkuu wa Taliban,Yousuf Ahmadi amethibitisha kuwa kundi lake ndio lilifanya shambulizi hilo na kwamba wamewaua askari polisi 12.Lakini hakuna ripoti huru iliyothibitisha madai hayo.