Wataliban wasema wameua mateka wa Kijerumani
21 Julai 2007Matangazo
Yousuf Ahmad anaesemekana kuwa ni msemaji wa Taliban, aliviarifu vyombo vya habari kwa njia ya simu kuwa mateka hao wa Kijerumani waliuawa baada ya kumalizika ule muda uliotolewa,kuanzisha moja kwa moja majadiliano pamoja na serikali za Ujerumani na Afghanistan.
Wataliban wanataka Ujerumani iwaondoshe wanajeshi wake 3,000 ambao ni sehemu ya vikosi vya NATO vinavyosimamia usalama nchini Afghanistan.
Wahandisi hao wawili wa Kijerumani na wafanyakazi wenzao watano wa Kiafghanistan,walitekwa nyara walipokuwa wakifanya kazi katika mradi wa bwawa nchini Afghanistan.