Watano washtakiwa kwa mauaji ya mlinzi wa amani Lebanon
2 Juni 2023Mahakama ya kijeshi ya Lebanon jana Alhamisi imewafungulia mashtaka watu watano kwa tuhuma za mauwaji ya mlinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka kutoka Ireland. Mkasa huo ulitokea Desemba mwaka jana.
Afisa mmoja ambae alizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina lake alisema watuhumiwa wote hao wanahusishwa na kundi la wanamgambo la Hezbollah la hukohuko Lebabon.
Mashtaka hayo yalifuatia uchunguzi wa nusu mwaka baada ya shambulio la msafara wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa karibu na mji wa Al-Aqbiya kusini mwa Lebanon,eneo ambalo linatajwa kuwa ni ngome ya Hezbollah.
Mashambulizi ya risasi yalisababisha vifo vya askari Seán Rooney, aliyekuwa na umri wa miaka 24, kutoka Newtown Cunningham huko Ireland, na mwenziwe Shane Kearney, wa umri wa miaka 22 alijeruhiwa vibaya.