1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Watano wauawa katika shambulizi la "kigaidi" nchini Uturuki

24 Oktoba 2024

Watu watano wameuawa katika shambulizi linalotajwa na serikali ya Uturuki kuwa ni la kigaidi kwenye Makao Makuu ya Kiwanda cha vifaa vya ndege cha nchini humo cha Turkish Aerospace.

uturuki Ankara 2024
Magari ya wagonjwa yakisubiri nje ya kiwanda cha vifaa vya ndege cha Uturuki cha Turkish Aerospace baada ya shambulizi, Oktoba 23, 2024Picha: AP/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya amesema washambuliaji wawili walivamia kiwanda hicho, na kuwaua watu hao na kuwajeruhi wengine 22, huku wawili wakiwa na hali mbaya.

Amesema washambuliaji hao waliuawa baada ya tukio hilo.

Amesema, washambuliaji hao huenda ni wa Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi kilichopigwa marufuku nchini humo, PKK.

Kufuatia shambulizi hilo, vikosi vya anga vya Uturuki vimeharibu vituo 32 vya PKK vilivyopo kaskazini mwa Iraq na kaskazini mwa Syria, hii ikiwa ni kulingana na wizara ya ulinzi usiku wa jana Jumatano na kuongeza kuwa wapiganaji wengi wa PKK waliuliwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW