Watano wauawa, maandamano yaendelea Misri
27 Januari 2011Matangazo
Mpaka sasa idadi ya waliouawa kwenye vurumai hizo imefikia watu watano akiwemo afisa mmoja wa polisi.Maelfu ya waandamanaji wanamtaka Rais Hosni Mubarak ajiuzulu baada ya kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 30.Kulingana na maafisa wa usalama wa Misri,kiasi ya watu 500 wanazuiliwa kwa sasa.Wakati huohuo,Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Guido Westerwelle,ameuelezea wasiwasi wake hususan kudumisha haki za raia wa Misri.Hali hiyo ya Misri inafanana na ile ya Tunisia kulikotokea maandamano yaliyoisababisha serikali kusambaratika mapema mwezi huu.