1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watapiamlo waongezeka Afrika:

26 Novemba 2003
ROMA: Idadi ya watu wanaoteseka kwa njaa inazidi kupanda duniani. Kufuatia ripoti ya Shirika la Chakula la wa Umoja wa Mataifa FAO, kwa jumla watu millioni 842 wanateseka kwa utapiamlo. Ni watu millioni 18 ziada kupindukia katikati ya miaka 90. Shirika FAO limedhukuru hasa hali inayotia wasiwasi barani Afrika, ambako kwa wasitani asilimia 30 ya waafrika wanasononeka kwa njaa. Wasiwasi zaidi ni katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kwani robo tatu ya wakaazi wana utapiamlo. Katika bara lote la Afrika, kwa mujibu wa ripoti hiyo, sababu ya njaa, ni ugonjwa wa ukimwi. Hadi mwaka 2020 wafanyakazi kama sehemu moja juu ya tano wa mashambani, linakisia shirika la FAO, wataugua ugonjwa huo, na uzalishaji wa mazao ya kilimo utazidi kupungua.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW