1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiTanzania

Watetezi wa haki wataka Polepole arejeshwe akiwa hai

7 Oktoba 2025

Watetezi wa haki za binadamu wamezitaka mamlaka za nchini Tanzania kuhakikisha kuwa mwanasiasa Humphrey Polepole anapatikana haraka tena akiwa hai huku sakata la kutekwa ama kupotea kwake likichukua sura mpya.

Tanzania | Bendera ya Tanzania | Bendera ya Taifa
Bendera ya Tanzania. Taifa hilo la Afrika Mashariki linajiandaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025Picha: imagebroker/IMAGO

Jeshi la Polisi Oktoba 7 pamoja na kusisitiza kuwa limeanza uchunguzi kuhusu kupotea kwa mwanasiasa Humphrey Polepole limesema linamtafuta ndugu wa Polepole, Augustino Polepole ili alisaidie jeshi hilo kuthibitisha shutuma alizotoa kuwa afisa wa Jeshi la Polisi alihusika katika tukio la utekwaji wa Humphrey Polepole.

Asasi za kiraia nazo zimeibuka na kuzitaka mamlaka hasa Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka kuchunguza tukio hilo. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kimesema iwapo Polepole anashikiliwa kwa tuhuma zozote basi mamlaka hazina budi kumfikisha mahakamani ili haki itendeke kwa mujibu wa sheria.

Humphrey azungumzia utekaji Tanzania

01:19

This browser does not support the video element.

Wakili wa Polepole aiandikia mahakama

Wakili Peter Kibatala ameaindikia mahakama ombi maalum kuitaka mahahama hiyo itowe amri ya dharura ya kutaka serikali kumpeleka Polepole mahakamani na ama kutoa sababu za kisheria za kumshikilia au Habas Corpus. Kibatala aliiandikia mahakama amri hiyo jana Oktoba 6 akieleza kuwa anazitaka mamlaka za raia kutoa taarifa juu ya usalama na maslahi ya kisheria ya Balozi Humphrey Polepole ambaye wakili huyo alimtambulisha kama mteja wake.

Uongozi wa CCM ambako Polepole amekuwa akisisitiza kuwa yeye bado ni mwanachama haukupatikana kuzungumzia sakata la kutoweka kwa mwanachama wao.

Siku ya Jumanne Tanzania iliamka na taarifa za kutekwa kwa mwanasiasa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba ambaye pia alikuwa akisimamia visiwa vya Karibiani, Amerika ya Kati, Columbia na Guetemala. Polepole ambaye baada ya kujiuzulu wadhifa wake wa ubalozi Julai mwaka huu aligeuka kuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya CCM, amewahi pia kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Mkuu wa Wilaya na Mbunge kwa nyakati tofauti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW