Watoa huduma usafiri wa umma wagoma Kampala
6 Julai 2022Kulingana na wadau katika sekta ya usafiri huo wa umma, hasa mabasi ya kwenda mikoani na mataifa jirani, wamezidi kupata hasara kutokana na idadi ndogo ya abiria wanaoweza kumudu gharama za nauli walizopandisha kutokana na bei ya mafuta.
Ni kutokana na sababu hii ndipo wameamua kusitisha huduma zao kwani hata mizigo ya kusafirisha imepungua.
Baadhi ya kamampuni za usafirishaji zimeiambia DW kwamba idadi ndogo ya abiria wanaumudu kusafiri mewalazimu kupunguza idadi ya magari ya abiria ili kwenda sambamba na hali halisi.
Soma pia:Museveni: Kupunguza ushuru kutavuruga mipango ya serikali
"Tumepunguza mabasi yetu kutoka tano hadi mawili kwa wiki wengine wamesimamisha shughuli zao" Alisema Jamal Mugisha ambae ni meneja wa kampuni ya mabasi ya Falcon.
Hali ya usafirishaji yatatizika
Kufuatia hatua ya baadhi ya mabasi kusitisha safari zao, wengi wa abiria walioathirika ni wafanyabiashara.
Hawawezi kupeleka au kuleta bidhaa kutoka vyanzo vyake na wamo mashakani ni lini hali itarejelea kawaida.
walisema biashara zao ambazo kwa kiwango kikubwa zinategemea usafirishaji wa bidhaa zimezorota kwa saa kadhaa tangu mgumo kuanza kwa mgomo huo wa wafanyakazi wa mabasi.
"Mambo ni magumu kwetu kutokana na nauli za juu na zaidi sasa usafiri umekuwa haba" Sam Kubo mfanyabiashara mjini Kampala aliiambia DW namna ambavyo biashara yake imeathirika kutokana na mgomo.
Hata kwa waendeshaji binafsi wa magari, bei ya mafuta imewalazimu kuegesha magari nyumbani na kuamua kutumia usafiri wa umma.
Hiki ndicho chanzo cha msongamano kupungua katika mji wa Kampala. Yunus Lubuuka ambaye ameaamua kutumia usafiri wa umma alisema kwa sasa hawezi kumudu kununua mafuta sababu ya bei ya sasa na kipato chake ni kidogo.
"Mimi siwezi kuimudu bei hii ili hali ninatakiwa kukidhi mahitaji ya familia afadhali niegeshe gari nitumie bodaboda"
Wafanyabiashara waishauri serikali
Kulingana na wafanyabiashara wa sekta ya usafiri, serikali pia inapoteza ushuru ambao ungetokana na kiasi kikubwa cha mafuta kuuzwa ikilinganishwa na sasa ambapo manunuzi yamepungua.
Soma pia:Karibu watu 20 wamekufa katika ajali ya barabarani Uganda
Hata hivyo hawako tayari kushirikiana wao wenyewe katika kujipunguzia gharama kwani kila kampuni inajitegemea katika kufanya biashara.
Ukilinganisha bei ya mafuta nchini Uganda ni ya juu kuliko mataifa jirani kama Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambazo bidhaa zake za mafuta hupitia Uganda.
Inadaiwa kuwa hili linasibishwa na kiwango cha juu cha ushuru ambao wadau wanapendekezaupunguzwe.