1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Watoa uamuzi wa mahakama kuanza kujadili kesi ya Trump

29 Mei 2024

Mawakili wa Donald Trump na waendesha mashitaka wa Manhattan wametoa hoja zao za mwisho jana kwa jopo la watoa uamuzi wa mahakama. Hukumu ya kesi hiyo itakuwa na umuhimu mkubwa kwa Trump na taifa la Marekani.

Trump katika mahakama wilaya ya Manhattan mjini New York
Mawakili wa Trump na waendesha mashitaka wamewasilisha hoja za mwisho katika kesi dhidi ya TrumpPicha: Spencer Platt/Getty/AP/picture alliance

Mwendesha mashitaka Joshua Steinglass amewaambia watoa uamuzi, kuwa Trump alishiriki katika njama ya kuwalaghai wapiga kura katika mwaka wa 2016. 

Kesi hiyo ya kihistoria, inahusu madai kuwa Trump na washirika wake walikula njama ya kuficha habari za kuwaaibisha wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka wa 2016 kwa kuwalipa watu akiwemo mcheza filamu za ngono aliyedai kuwa yeye na Trump walifanya mapenzi muongo mmoja uliotangulia.

Naye wakili wa Trump Todd Blanche alisema hakuna yeyote kati ya mchezafilamu huyo, Stormy Daniels wala mwanasheria wa Trump aliyemlipa mwanamke huyo, Michael Cohen, anayeweza kuaminiwa.

Soma pia: Trump apandishwa kizimbani kujibu kesi ya jinai

Amesema rais Trump hana hatia, kwa sababu hakufanya uhalifu wowote, na mwendesha mashitaka hakuweza kuthibitisha kikamilifu mashitaka hayo. Ikiwa ni chini ya miezi sita kabla ya uchaguzi ambao Trump anatafuta kurejea katika Ikulu ya White House, umuhimu wa hukumu ya kesi hiyo ni mkubwa kwa Trump mwenye umri wa miaka 77 na kwa Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW