1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto 2,000 hufa kila siku kwa uchafuzi wa hewa - Ripoti

19 Juni 2024

Ripoti iliyotolewa na taasisi moja inayoshughulikia na athari za kiafya yenye makao yake Marekani, inasema karibu watoto 2,000 hufariki kila siku kutokana na matatizo ya kiafya yanayofungamanishwa na uchafuzi wa hewa.

Moshi wa viwandani
Moshi kutoka viwandani unaochafua hali ya hewa.Picha: Pond5 Images/IMAGO

Taasisi hiyo inasema uchafuzi wa hewa ulichangia vifo vya watu milioni 8., ikiwa ni asilimia 12 ya vifo vyote vilivyotokea duniani katika mwaka wa 2021.

Zaidi ya vifo 500,000 katika hivyo vinadaiwa kusababishwa na matumizi ya nishati chafu ya kupikia kama mkaa, mbao au kinyesi cha ng'ombe na vilitokea hasa kwenye mabara ya Afrika na Asia.

Soma zaidi: WHO: Gaza bado inakabiliwa na kitisho cha njaa

Ripoti hiyo inasema uchafuzi wa hewa kwa sasa ndio sababu ya pili kubwa ya vifo vya mapema kote duniani.

Hii ina maana kwamba uchafuzi wa hewa sasa umevuuka matumizi ya tumbaku na ulaji mbaya na inashikilia nafasi ya pili baada ya shinikizo la damu kama sababu kuu ya kwanza ya vifo vya mapema duniani. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW