1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto 30 waishi magerezani nchini Kenya

Admin.WagnerD31 Januari 2023

Watoto 300 wanaishi katika magereza pamoja na wazazi wao wanaotumikia vifungo nchini Kenya huku serikali ya Kenya ikishinikiza mageuzi katika mfumo wa magereza ili kukabiliana na changamoto za watoto hao.

Kenia Wahlen
Picha: DW/Shisia Wasilwa

Pamoja na hilo, serikali pia inalenga kukabiliana na unyanyapaa na madhila wanayopitia wafungwa wanaporejea nyumbani. 

Katika ziara yake kwenye magereza yaliyoko mjini Nakuru, katibu mkuu wa magereza nchini Mary Muthoni ameelezea wasiwasi kuhusu idadi kubwa ya watoto walio chini ya umri wa miaka minne wanaoishi kwenye magereza pamoja na mama zao, kama anavyoelezea hapa, "Mtoto ambaye hajatenda uhalifu wowote. Mtoto ambaye amezaliwa gerezani. Mtoto ambaye analala katikati ya wafungwa. Mtoto huyu yuko kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa. Mtoto huyu anakabiliwa na unyanyapaa kwa kuzaliwa gerezani au kuishi gerezani kwa muda mrefu. Nchini kote tuna watoto 300 wanaoishi magerezani. Hiyo ni idadi kubwa. Hao ni watoto ambao bado wananyonya ama walio na mahitaji maalum.”

Wafungwa katika gereza ya Athi River nchini Kenya wakiwa wanasubiri kupata chakula cha jioni.Picha: picture-alliance/dpa/D. Kurokawa

Afisa huyu mkuu anaeleza kuwa baadhi ya kina mama hao pia wana watoto wengine nyumbani na inabidi wapelekwe kwenye makaazi ya watoto yatima ndiposa mama aweze kutumikia kifungo chake. Hali hii anasema inamkosesha mtoto maadili ya kifamilia. Hata hivyo, anaamini kuwa ni jambo linaloweza kurekebishwa kupitia mtazamo wa kibinaadamu kwenye mageuzi ya kisheria.

"Tunashirikiana na mahakama na tumekubaliana kufanya kazi pamoja kuhakikisha kwamba tunapunguza msongamano kwenye magereza. Njia moja ya kufanikisha hili ni kuhakikisha kwamba kesi za wahalifu waliofanya makosa madogo na za kinamama walio na watoto wadogo zinaangaliwa upya. Kwa mfano, kama wameshtakiwa kwa makosa madogo, wanaweza kuhukumiwa kifungo cha kuhudumu katika jamii," aliongezea afisa huyo.

Pamoja na hayo, maafisa wakuu wa magereza nchini na wadau wengine wanahimiza kuunganishwa tena kwa wafungwa kwenye jamii wanapokamilisha kutumikia kifungo gerezani, huku wakisisitiza hitaji la wafungwa kupewa mafunzo ya kiufundi kuwawezesha kujisimamia wanapotoka gerezani. David Macharia msimamizi wa kitengo cha ustawi wa wafungwa kwenye gereza kuu la Nakuru anaeleza.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW