1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto 50 kati ya 300 waliotekwa wawatoroka watekaji Nigeria

23 Novemba 2025

Wanafunzi 50 kati ya 300 waliotekwa nyara na watu waliojihami kwa silaha katika shule ya Kikatoliki ya Mtakatifu Mary, iliyopo kwenye jimbo la katikati mwa Nigeria la Niger, wamefanikiwa kuwatoroka watekaji wao.

Nigeria |Watoto 50 kati ya 300 wawatoroka watekaji wao
Watoto 50 kati ya 300 waliotekwa wawatoroka watekaji wao NigeriaPicha: Ben Curtis/AP Photo/dpa/picture alliance

Kulingana na Chama cha Kikristo cha Nigeria, watoto hao waliotoroka kati ya Ijumaa na Jumamosi tayari wameungana na wazazi wao.

Zaidi ya wanafunzi 300 wenye umri kati ya miaka 8 na 18 na waalimu 12 walitekwa nyara na watu hao wasiojulikana hali inayowapa hofu raia wa taifa hilo.

Mamlaka zimesema vikosi maalumu vimeshaanza kufanya msako wa kujaribu kuwaokoa wanafunzi hao lakini haijataja idadi kamili ya waliotekwa.

Hili ni tukio la pili la aina hiyo ndani ya wiki moja baada ya wanafunzi wengine 25 kutekwa nyara katika jimbo la Kebbi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW