UNICEF: Watoto 68,000 wanahitaji msaada wa kiutu Nepal
12 Februari 2024Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema watoto wapatao 68,000 na familia zao ambao walinusurika kwenye tetemeko baya zaidi la ardhi kutokea Nepal katika kipindi cha takribani miaka minane iliyopita wanahitaji msaada zaidi wa kibinadamu ili kustawisha upya maisha yao. Shirika hilo limesema ikiwa imetimia siku 100 baada ya tetemeko hilo ambalo takriban watu 200,000 wakiwemo watoto 68,000. wanakabiliwa na baridi kali katika makazi ya muda. Na wengi wao wenye kukabiliana na baridi wakihitaji msaada wa kiutu. Shirika la Umoja wa Mataifa limetoa himizo la ombi la mchango wa dola milioni 14.7 kikiwa kiwango mahususi cha fedha za kusaidia watoto hao. Novemba 3, tetemeko la ardhi la kiwango cha 6.4 katika kipimo cha richter lilikumbawilaya mbili za Jajarkot na Rukum katika eneo la magharibi la Himalaya na kuua takrian watu 154, nusu ya hao wakiwa ni watoto.