1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto wa majiani Sierra Leone

15 Septemba 2009

nani anawasaidia ?

Miaka 10 baada ya kumalizika vita vya kienyeji nchini Sierra Leone, nchi hii ingali ikipambana na shida za athari za vita hivyo.Wahanga wengi ni watoto na chipukizi ambao kati yao, maalfu bado wanaishi majiani.

Tangu mwongo mmoja kupita, alao rasmi amani imerejea Sierra Leone, lakini kwa wakaazi wake wengi ,bado hawaioni.Mzigo mzito wa vita vile, ni kuselelea umasikini zaidi. Tena katika nchi ambako thuluthi-mbili ya wakaazi wake, ni vijana wa chini ya umri wa miaka 25.Miongoni mwa waliopoteza katika vita hivyo , ni kizazi kizima cha umri kati ya miaka 17-25. Kizazi hiki kina matumaini gani ya maisha bora ? Susan's Bay,ni mtaa wa masikini wa jiji kuu Freetown.

Njia kuelekea Susan's Bay inaongoza kupitia sokokoni.Katika soko hilo kuna ndoo za plastik na suruali za kufanyia mazowezi ya kukimbia za bei nafuu mbali na matunda na mboga-mboga.Ni sura ya kawaida barani Afrika.Huoni alama za vile vita vya kienyeji katika vichochoro vyembamba vinavyoongoza hadi baharini.

Huko ukingoni mwa bahari katika vibanda vya mbao na mabati vya mtaa wa masikini wa Susan's Bay,vita vya kienyeji kana kwamba vyakaribia kuripuka upya. Zaidi ya watu 50.000 walifariki dunia katika vita vya kienyeji na hapa hasara za vita vile ziko dhahiri kujionea.Wazi kabisa ni ufukara mkubwa .Isitoshe, kuna alama za ukatili uliopita na wa kutisha.Mfano ,ni watu kujikuta hawana wenzao na wako pekee.

Hata watoto wadogo na chipukizi, wanaonekana wameghadhibika.Mfano, mtoto wa miaka 8 anaechota maji anaepiga zumari lake manjano kunadi maji anayotembeza kuuza. Au msichana aliebeba mzigo mzito wa kuni anaebidi kupita njia yenye daraja mbali mbali za kupanda akipita kundi la watu.Hakuna mengi hapa ya kukufanya ucheke au ufurahi katika mtaa huu wa nchi masikini labisa ya dunia hii.

Taka zinatupwa kwenye misingi ya maji inayopitia mtaa huo. kandoni mwa vibanda vya mbao kuna mahala anakwenda mara nyingi mtumishi wa shughuli za usaidizi aitwae Raymond: Anasema,

"Hapa ni maskani ya watoto ambao wanaoshi majiani.Wanaishi kwa kuuza madawa ya kulevya au kwa wizi.Wanalala pia hapa .Serikali haiwatazami kwa njia yoyote.na hakuna anaewaangalia."

Hip Hop anatujia.Ni kijana mrefu mwenye umri wa miaka 17 akivaa mtndo wa cowboy.Yeye ni miongoni mwa watoto wa majiani 3000 wa jiji la freetown.Kifo cha Michael Jackson kimemuumiza sana.Lakini ukimuuliza matatizo yake binafsi, basi anakwepa kwepa:

"Nimekutana na baba yangu (lakini alikataa kunichukua nyumbani.).."

Kijana huyu Hip Hop alikimbia nyumbani kwao karibu na mwisho wa vita vya kienyeji.Hajui kusoma wala kuandika.Kwani hajenda shule.Miaka 10 ya kuwa majiani yamemfanya kuchoka lakini hakusahau ndoto yake:Ataka kuwa nyota ya muziki wa pop kama vile kipenzi chake Michael Jackson.Akisimulia hayo,hucheka binafsi.

"Kuendesha Taxi ya piki-piki au kutengeza magari yalioharibika."

Mtumishi wa shughuli za usaidizi Raymond anamjua Hip-Hop muda mrefu.Raymond na shirika lake la misaada "christian Brothers"-ndugu wa kikristu anajaribu kuwasiliana na ukoo wa kijana huyu.Lakini anakumbana na tatizo lile lile mara kwa mara.

Inakupasa kujionea hali wanazoishi wazee wa watototo hawa.Jinsi waliovyo mafukara hawamudu kuwahudumia watoto wao.Na hii ndio sababu baadhi yawakati ni shida kuwarejesha watoto hao kwa familia zao....Wiki iliopita tulifanikiwa kumrejesha mtoto mmoja kwa familia yake huko Maschaka,si mbali sana kutoka mji mkuu Freetown.Tukaahidiana na wazee wake kwamba tutabeba gharama za mwaka mzima za masomo yake ili aweze kwenda shule.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW