1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto wa mitaani waimba "rap" ili kujikimu, DRC

18 Juni 2023

Licha ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwa na utajiri mkubwa wa madini ulimwenguni, lakini takriban theluthi mbili ya watu wake wanakabiliwa na umasikini mkubwa, wakiishi chini ya kipato cha dola 2.15 kwa siku.

DR Kongo Kinshasa Verkehr
Picha: Dirke Köpp/DW

Vijana na watoto wanaoishi mitaani ni changamoto nyingine inayolikabili taifa hilo la hsa katika mji mkuu Kinshasa, ingawa baadhi wanaamua kufanya shughuli zitakazowaongezea kipato. 

Soma Zaidi: DRC yasema haitaruhusu madini yake kuchakatwa nje ya Afrika

Maisha ya mitaani ni ya kusikitisha na ya kukatisha tamaa, anasema kijana asiye na makazi anayeishi katika mji mkuu w Kishansa, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, aliejiita "Biashara". Kijana huyo wa miaka 19 mwenye matamanio makubwa, ni mmoja wa vijana kadhaa wasio na makazi ambao wamepata kimbilio katika muziki wa kufokafoka.

Anasema mwili wake na wenzake huonekana iliyochoka mno kutokana mapambano ya kila siku lakini yasiyoleta tija kubwa.

Vijana hawa hujifunza muziki kupitia kituo kidogo cha sanaa cha Mokili Na Poche, kilichopo katika mtaa unaokaliwa na wafanyakazi wa Bandalungwa, ambacho huwasaidia watoto wa mitaani na vijana huko Kinshasa, ambao wametelekezwa ambao kulingana na mashirika ya misaada wanafikia 20,000.

Huko Kinshasa, vijana hawa huitwa "Shegue" na wengi hujikuta wakishia kurandaranda mitaani kutokana na umasikini mkubwa ama familia zao kushutumiwa kuwa washirikina.

Ajira kwa vijana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni tatizo kubwa linalowasukuma baadhi kujihusisha na shughuli nyingine kama sanaa. Picha: Dirke Köpp/DW

Maisha yao mara nyingi hugubikwa na vurugu, na wengi wao hutumia dawa za kulevya na wengine wakifaanya ukahaba, huku raia wengi nchini humo wakiwa hawana amani na watoto ama vijana hawa.

Lakini kituo cha Mokili Na Poche, kilichofunguliwa Novemba mwaka jana, kinalenga kuhamasisha vijana waliotelekezwa na wasio na makazi kugeukia shughuli za ubunifu kama vile kutengeneza bidhaa za mifuko kwa kutumia plastiki zilizotumika au kufanya muziki.

Biashara ama jina lake halisi Juniro Mayamba Ngatshwe, ana matamanio kama ilivyo kwa wenzake kutumia fursa yoyote inayojitokeza mbele ya uso wake.

Chadrack Mado, kijana mwingine anayeishi mtaani, alisema anakuja kituoni hapo ili baadaye asije kuitwa "luna" neno linalotumiwa na wenyeji wakimaanisha kundi la majambazi sugu wa Kinshasa wanaotumia mapanga kufanya uhalifu.

Alisema "Kijana wa mtaani: Ninakuja hapa kujifunza kwa ajili ya maisha yangu ya baadaye na kwa manufaa yangu mwenyewe, ili kesho nisije kuwa jambazi au mwizi, na badala yake jamii inikubali," 

Cedrick Tshimbalanga, mkurugenzi wa kampuni ya Mokili Na Poche, anaeleza jinsi vurugu na hali ya kukata tamaa vilivyotawala maisha ya vijana wanaoishi mtaani mjini Kinshasa. Anasema hawa wote wana viwembe mifukoni kwa ajili ya kujilinda na kuongeza kuwa wapo wengine ambao hakaa siku kadhaa bila ya hata kula.

Ajira kwa vijana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni tatizo kubwa linalowasukuma baadhi kujihusisha na shughuli nyingine kama sanaa. Picha: Dirke Köpp/DW

Soma Zaidi:Marekani yaiomba DRC kuondoa vitalu vya mafuta kwenye mnada 

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa madini. Takriban theluthi mbili ya idadi ya watu milioni 100 nchini humo wanaishi chini ya dola 2.15 kwa siku, hii ikiwa ni kulingana na Benki ya Dunia.

Studio hiyo mpya ya kurekodia inawasaidia wale wanaopenda muziki miongoni mwa vijana wanaotembelea Mokili Na Poche.

"Biashara” anasema ndoto yake ilikuwa ni kufuata nyayo za wakali wa muziki wa Kongo kama vile Fally Ipupa, kuendesha gari zuri na kwenda Marekani kutembea. Anasema maisha ya mtaani ni magumu, na hasa akiangazia jinsi baadhi ya vijana kama yeye wasio na makao walivyokuwa wakimuunga mkono lakini wengine walijaribu kumdidimiza. Lakini hata hivyo akasema muziki uko kwenye damu yake, kwa hiyo hakukubali kuvunjwa moyo.

Kongo ina utajiri mkubwa wa muziki na baadhi ya makundi, kama vile Staff Benda Bilili, ya watu wenye ulemavu, yameipata umaarufu kuanzia mitaa ya Kinshasa hadi kimataifa. Vijana kadhaa wa Mokili Na Poche tayari wamerekodi albamu, na mwanamuziki mmojaa mkubwa, ingawa hawakulipwa chochote.

Vijana hawa ambao wengi wao wana alama za majeraha kwenye miili yao, huimba miziki yenye ujumbe mkali lakini usiohamasiha mapambano. Wengine hata hawajui umri wao, lakini kikubwa wanachokitaka ni kukabiliana na namna jamii inavyowachukulia.

Kituo hicho kimeanza kutengeza albamu ya nyimbo za kufokafoka na mmoja wao anasema muziki unawatia moyo wa kusonga mbele.

Sikiliza Zaidi: 

DRC yaanza hatua kuishtaki Rwanda ikidai inapora madini yake

This browser does not support the audio element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW