1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 10 wafa kwa kugongwa na gari kimakusudi nchini Canada

Zainab Aziz
24 Aprili 2018

Polisi mjini Toronto wamemtambua dereva aliyewauwa watu 10 pale kwa gari lake. Watu hao walikuwa wanatembea kandoni mwa barabara katika muda wa saa za mchana. Watu wengine 15 walijeruhiwa kwenye mkasa huo. 

Kanada Wagen rast in Menschen auf einer Kreuzung in Toronto
Picha: picture-alliance/AP Photo/The Canadian Press/A. V. Elkaim

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema shambulio hilo ni baya na la kijinga, ni moja ya mashambulizi ya kutisha zaidi katika historia ya karibuni ya Kanada.

Waziri Mkuu Trudeau ameonyesha huruma zake kwa wale wanaohusika na mkasa uliotokea. Amesema raia wote wanapaswa kujisikia wako salama kutembea katika miji na miongoni mwa jamii. Bwana Trudeau amesema hali hii inafuatiliwa kwa ukaribu, na kwamba Canada itaendelea kufanya kazi na vyombo vya usalama nchini kote kuhakikisha usalama wa wananchi wake.

Waziri mkuu wa Canada Justin TrudeauPicha: picture alliance/AP Photo/A. Vaughan

Waziri wa usalama wa umma nchini Canada Ralph Goodale amesema shambulio hilo ni baya na la kutisha lakini halihusiani na vitendo vya kigaidi. Waziri Goodale, amesema nchi yake haijabadili  tahadhari katika kiwango cha mashambulizi ya kigaidi. Waziri wa usalama wa umma nchini Kanada Ralph Goodale amesema shambulio hilo ni baya na la kutisha lakini halihusiani na vitendo vya kigaidi. Waziri Goodale, amesema nchi yake haijabadili tahadhari katika kiwango cha mashambulizi ya kigaidi.

Taarifa ya polisi

Mkuu wa polisi mjini Toronto amethibitisha kuuwawa kwa watu hao 10 na wengine 15 waliojeruhiwa.  Duru za hospitali ya Sunnybrook zimefahamisha kwamba baadhi ya majeruhi wamo katika hali mbaya. Mkuu wa polisi amemtaja mshambuliaji kuwa ni Alek Minassian mwenye umri wa miaka 25, alikuwa anaishi katika kitongoji cha Richmond Hill. Bwana Saunders amesema Minassian hakuwa ni mtu aliyekuwa anatambulika na polisi kwa kuhusika na vitendo vya aina yoyote vyenye kutia mashaka. Na taarifa kutoka kwenye mitandao ya kijamii zinasema kijana huyo ni mwanafunzi wa chuo kikuu.

Mkuu wa polisi nchini Canada Mark SaundersPicha: picture-alliance/AP Photo/The Canadian Press/N. Denette

Ni tukio la makusudi

Mkuu huyo wa polisi aliwaambia waandishi wa habari kwamba dalili zinaonyesha wazi mtu huyo alitenda kosa hilo kwa kudhamiria, ameeleza pia dereva huyo alijaribu kukimbia lakini polisi walifanikiwa kumkamata na kwa sasa anashikiliwa katika kituo cha polisi na kwamba polisi wanachunguza kiini cha kufanyika kwa shambulio hilo. Bwana Mark Saunders amefahamisha kwamba mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani baadae leo.

Tukio hilo limefanyika wakati ambapo mawaziri wa mambo ya nje kutoka kundi la nchi saba zinazoongoza kiviwanda duniani wanapokutana huko nchini Canada kujadili masuala ya kimataifa katika matayarisho ya mkutano wa kilele wa viongozi wa kundi la nchi hizo saba utakaofanyika mwezi Juni. Waziri wa Usalama wa umma wa Canada bwana Ralph Goodale amesema mawaziri hao wameelezea masikitiko yao.

Mwandishi:Zainab Aziz/APE/RTRE

Mhariri: Iddi Ssessanga