1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSudan

Watu 10 wafariki baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka Sudan

31 Machi 2023

Wafanyakazi wapatao 10 wamefariki dunia baada ya machimbo ya mgodi wa dhahabu kuporomoka kaskazini mwa Sudan

Goldmine Sudan Wüste Khartum
Picha: Ashraf Shazly/AFP/Getty Images

Shirika la habari la serikali, SUNA, limeripoti kuwa wafanyakazi hao wamekufa baada ya paa la mgodi wa dhahabu wa Jebel Al-Ahmar kuporomoka jana.

Wachimbaji wengi bado hawajulikani walipo. Kwa mujibu wa SUNA, miili kadhaa, wengi wao wakiwa vijana wa kiume, imepatikana kutoka kwenye eneo la tukio na juhudi za uokozi bado zinaendelea.

Mgodi huo wa dhahabu uko karibu na mpaka wa Misri. Kuporomoka kwa migodi ya dhahabu Sudan ni jambo la kawaida, ambako viwango vya usalama na matengenezo ni duni.

Mnamo mwaka 2021, watu 31 walikufa baada ya machimbo ya dhahabu kuporomoka kwenye jimbo la Kordofan Magharibi. Sudan ni mchimbaji mkubwa wa dhahabu na madini mbalimbali yaliyoko nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW