1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 10 wafariki katika shambulizi la soko la hisa Pakistan

29 Juni 2020

Watu wasiopungua 10 wakiwemo magaidi wanne wameuawa katika shambulio dhidi ya soko la hisa la Pakistan, lililoko katika mji wa bandari wa Karachi.

Pakistan Karatschi | Angriff auf die Börse
Picha: Reuters/A. Soomro

Kamanda wa polisi wa kanda Sharjeel Kharal, ameviambia vyombo vya habari kwamba walinzi wanne wa usalama, afisa mmoja wa polisi na raia mmoja ni miongoni mwa waliouawa. Ameongeza kwamba magaidi wote wanne wameuawa, na kwamba watu wengine saba, wakiwemo askari polisi watatu wamejeruhiwa katika shambulio hilo. Mkurungenzi Mtendaji wa soko la Hisa la Pakistan Farrukh Khan, amesema shambulio hilo lilikuwa zito, lakini kwa bahati nzuri magaidi hawakuweza kuingia eneo kuu la jengo la soko hilo. Zaidi ya wafanyabiashara na wafanyakazi 1,000 walikwepo katika jengo wakati wa shambulio kwa mujibu wa ripoti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW