1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUlaya

Watu 10 wamekufa baada ya kimbunga kupiga Ukraine

28 Novemba 2023

Watu 10 wamekufa na wengine 23 wamejeruhiwa kutokana na kimbunga na kuanguka kwa theluji nchini Ukraine na kuongeza shinikizo kwa hospitali na gridi ya mfumo wa umeme ambao umelemewa kutokana na uvamizi wa Urusi.

Ukraine | Majengo yaliokuwa makazi ya raia yakiwa yameharibiwa
Majengo yaliokuwa makazi ya raia yakiwa yameharibiwa vibaya UkrainePicha: Aris Messinis/AFP

Waziri wa mambo ya ndani Ihor Klymenko ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii kuwa, majeruhi hao 23 wakiwemo watoto wamejeruhiwa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Upepo na dhoruba kali iliipiga upande wa kusini mwa Ukraine tangu Jumapili na kukatiza huduma za umeme na kufunga barabara.

Soma pia: Watu nusu milioni Crimea hawana huduma ya umeme

Klymenko ameongeza kuwa, jumla ya nyumba 411 katika mikoa 11 zimepoteza umeme na kuwa zaidi ya magari 1,500 yameokolewa.


 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW