Watu 10 wauawa DRC kufuatia shambulizi la ADF
8 Januari 2019Matangazo
Kiasi ya raia wanane ikiwa ni pamoja na jamaa za wanajeshi wameuwawa katika mashambulizi yaliyofanywa usiku na watu wenye silaha katika eneo tete la mashariki mwa Congo, jeshi limesema leo.
Watu wanane wameuwawa ikiwa ni pamoja na wanne ambao ni ndugu wa wanajeshi, katika wilaya ya Mavivi kaskazini mwa eneo la Beni, msemaji wa jeshi wa jimbo hilo Mark Hazukay ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.
Polisi imeweka idadi ya waliouwawa kuwa ni 10, baada ya hapo kabla kutangaza kuwa waliouwawa ni wanane.