1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 10 wauawa katika shambulio la ADF mashariki mwa Kongo

11 Agosti 2024

Takriban watu 10 wameuawa jana katika mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na kundi la waasi la ADF mashariki mwa Kongo.

Demokratische Republik Kongo Soldaten
Wanajeshi wa Kongo wakipiga doria wakati wa operesheni ya kijeshi dhidi ya makundi yenye silaha eneo la Beni, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Picha: Alain Uaykani/Xinhua/IMAGO

Mashambulizi hayo yametokea katika eneo la Beni, jimbo la Kivu Kaskazini.

Kiongozi wa mashirika ya kiraia Kinos Katuo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, wapiganaji wa ADF walivamia eneo la Beni mapema jana asubuhi.

Chifu wa eneo hilo Leon Siviwe amethibitisha vifo vya watu hao, wakiwemo wanaume na wanawake.

Soma pia: Watu 42 wauwawa na waasi wa ADF nchini Kongo

Mtu mmoja aliyenusurika kifo amesema nyumba zao zimeteketezwa kwa moto wakati wa mashambulizi hayo.

Waasi wa ADF wenye mafungamano na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu pia limelaumiwa kwa kuhusika na shambulio lililosababisha vifo vya watu 20 mwishoni mwa mwezi uliopita.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW