1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 10 wauawa kwa kisu Canada, 15 wajeruhiwa

5 Septemba 2022

Polisi nchini Canada inawasaka washukiwa wawili katika tukio ambalo watu kumi waliuawa kwa kuchomwa kisu na wengine karibu 15 kujeruhiwa katika eneo moja la jamii ya kiasili lisilo na wakaazi wengi

Kanada Messerstechereien | PK Kommissarin Rhonda Blackmore
Picha: Michael Bell/The Canadian Press/AP Photo/picture alliance

Polisi nchini Canada inawasaka washukiwa wawili katika tukio ambalo watu kumi waliuawa kwa kuchomwa kisu na wengine karibu 15 kujeruhiwa katika eneo moja la jamii ya kiasili lisilo na wakaazi wengi. Mauaji hayo ya watu wengi ndio makubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya karibuni nchini Kanada.

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema mashambulizi hayo katika eneo la Saskatchewan ni ya kutisha na ya kuvunja moyo. Polisi imewataja washukiwa wawili Damien Sanderson mwenye umri wa miaka 31, na Myles Sanderson mwenye umri wa miaka 30, na kutoa picha zao na maelezo lakini hakuna taarifa zaidi kuhusu nia yao wala kuhusu wahanga.

Polisi ya Saskatchewan imesema inaonekana kuwa baadhi ya wahanga huenda walilengwa na wengine walishambuliwa bila mpangilio.

Maelezo zaidi yatafuata......

afp, reuters

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW