Watu 100 wahofiwa kufa kutokana na mvua kubwa Somalia
11 Novemba 2013Taarifa za awali zinaonyesha kuwa makazi, majengo, boti na vijiji vizima vimehariwa na mifugo zaidi ya 100,000 wameangamia, hivyo kuhatarisha kipato cha maelfu ya wa wakaazi wa eneo hilo. Serikali imesema mvua kubwa na upepo mkali vinatarajiwa kuendelea hadi Jumatano wiki hii.
Habari zilizokusanywa kutoka maeneo ya pwani kupitia mawasiliano ya kawaida ya simu katika kipindi cha saa 48 zilizopita, zinaonyesha kuwa hadi watu 100 huenda wameuawa , wakati mamia ya watu wengine hawajulikani waliko.
Rais wa eneo linalojitawala la Puntland Abdirahman Mohamed Farole amesema "mzozo huo ni mkubwa" huku serikali ikitangaza hali hiyo kuwa ni janga. Serikali inaendelea na shughuli za kusambaza misaada ya dharura kwa walioathirika, lakini pia imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kutoa mchango wao. Mvua kubwa pamoja na upepo mkali unatarajiwa kuendelea kulikumba eneo hilo hadi Jumatano wiki hii.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohammed Khelef