1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 11 wajeruhiwa Kharkiv kufuatia shambulio la Urusi

8 Oktoba 2024

Watu 11, akiwemo mtoto, wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi ya Urusi katika mji wa Kharkiv kaskazini mashariki mwa Ukraine.

Uharibifu baada ya shambulio la anga la Urusi huko Kharkiv
Wafanyakazi wa dharura wanaonekana mbele ya jengo la ghorofa lililokumbwa na shambulio la anga la Urusi mjini Kharkiv, Ukraine Oktoba 2, 2024.Picha: Vitalii Hnidyi/REUTERS

Gavana wa eneo hilo, Oleh Syniehubov, amesema kupitia mtandao wake wa kijamii wa Telegram kwamba shambulio hilo limeharibu pia miundombinu kadhaa na kwamba kwa sasa wanaendelea na uchunguzi ili kufahamu zana zilizotumiwa.Jeshi la Ukraine limesema limedungua droni 18 za Urusi na kushambulia maeneo yanayokaliwa kimabavu ya Crimea ambapo zaidi ya wakazi 1,000 wamehamishwa kutokana na moto uliozuka katika kituo kikubwa cha mafuta.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW