1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

India: Watu 11 wafa baada ya kuvuta hewa ya gesi iliyovuja

30 Aprili 2023

Watu 11 wamekufa baada ya kuvuta hewa ya gesi iliyovuja katika mji wa Ludhiana kwenye jimbo la Punjab kaskazini mwa India.

Indien | Gasleck in Giaspura, Ludhiana, Punjab
Picha: National Disaster Response Force/AP Photo/picture alliance

Watu 11 wamekufa baada ya kuvuta hewa ya gesi iliyovuja katika mji wa Ludhiana kwenye jimbo la Punjab kaskazini mwa India. Mbunge wa jimbo hilo ameeleza kuwa watu wengine tisa wamelazwa hospitalini kutokana na kadhia hiyo iliyotokea kwenye eno la viwanda. Kikosi cha kukabiliana na maafa nchini humo kipo kwenye eneo la tukio pamoja na wataalam wengine ili kutathmini chanzo kilichosababisha kuvuja kwa gesi hiyo. Maafisa wa polisi wanaendelea kupiga doria huku wakiwataka wenyeji kutosogelea eneo hilo. Waziri Mkuu wa jimbo la Punjab Bhagwant Mann amesema gesi hiyo ilivuja kutoka kiwandani lakini hakutoa maelezo zaidi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW