Watu 11 wauawa mashariki mwa DRC
4 Februari 2019Matangazo
Kiasi ya watu 11 wameuawa katika mapigano yaliyotokea kati ya wanajeshi na wapiganaji wa kundi lenye silaha ambalo halijulikani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Taarifa hiyo imetolewa jana jioni na jeshi la Kongo. Msemaji wa jeshi katika jimbo la Ituri, Jules Ngongo, amesema watu wengine sita walijeruhiwa wakati mapigano hayo yalipozuka kwenye mji wa Torgess katika jimbo hilo.
Ngongo amesema miongoni mwa waliouawa ni raia watatu, wanajeshi wawili na waasi sita, huku waasi wengine sita wakiwa wamejeruhiwa.
Makundi kadhaa ya waasi yanaendesha operesheni zake mashariki mwa Kongo, yakigombania kuhusu eneo hilo lenye utajiri wa rasilimali za madini.