1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 11,000 wakimbia makaazi yao kusini magharibi mwa Niger

13 Julai 2023

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na mamlaka ya ndani ya Niger, takriban watu 11,000 wameyakimbia makaazi yao Kusini Magharibi mwa nchi hiyo mnamo mwezi huu.

Niger - Migranten
Picha: Désirée von Trotha/picture alliance

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kiutu (OCHA) mjini Niamey imesema watu hao wanakimbia machafuko yanayofanywa na makundi ya watu wenye silaha.

Ghasia hizo zinatokea kwenye mkoa wa Tillaberi na eneo la mpaka unaozikutanisha nchi tatu za Niger, Burkina Faso na Mali.

Soma zaidi: Mamia ya watu waathirika na mafuriko na kipindupindu huko Cameroon na Chad

OCHA imesema watu waliyakimbia makaazi yao baada ya mauaji ya wanakijiji wawili usiku wa Julai 3.

Baadhi yao walilazimika kulala kwenye vyumba vya madarasa na wengine walihifadhiwa na familia zingine.

Niger imekumbwa na uasi wa wanamgambo wenye itikadi kali wanaofanya mauaji na kuwateka raia. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW