MigogoroMashariki ya Kati
Watu 12 wauawa kufuatia shambulio la Israel Gaza
9 Januari 2025Matangazo
Wasichana watatu na baba yao waliuawa baada ya shambulio la anga la Israel kuilenga nyumba yao katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, katikati mwa Gaza.
Katika shambulio lingine tofauti, watu wanane waliuawa baada ya nyumba yao kushambuliwa katika mji wa Jabalia, kaskazini mwa Gaza, sehemu ambayo jeshi la Israel limeelekeza oparesheni yake tangu Oktoba 7.
Mashambulizi hayo ya hivi karibuni yametokea wakati Qatar, Misri na Marekani zikiongoza mazungumzo mjini Doha, kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas ili kufikia makubaliano ya kumaliza mapigano Gaza yaliyodumu miezi 15.