1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Watu 127 wauawa kufuatia mapigano nchini Sudan

11 Desemba 2024

Watu wasiopungua 127 wengi wao wakiwa raia, wameuawa nchini Sudan kufuatia mapigano ya hapo jana kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF.

Basi la abiria lililoteketea kwa moto kufuatia mashambulizi huko Omdurman
Basi la abiria lililoteketea kwa moto kufuatia mashambulizi huko OmdurmanPicha: Khartoum State Government/REUTERS

Karibu watu 60 wameuawa katika mji wa Omdurman huku wengine zaidi ya 100 wakiuawa katika soko la Kaskazini mwa mji wa Kabkabiya huko Darfur.

Gavana wa Khartoum, Ahmed Othman Hamza, amesema kombora lililorushwa na  RSF lilipiga basi la abiria na kuwaua watu wote 22 waliokuwamo ndani.

Pande hizo mbili ambazo zimekuwa zikipambana tangu Aprili mwaka 2023, zimeshutumiwa kushambuliana vikali kwa makombora na kuyalenga maeneo ya raia yanayokaliwa na watu wengi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW