Watu 13 wadaiwa kuuawa na wanamgambo wa RSF nchini Sudan
4 Novemba 2024Chanzo kimoja kilichozungumza kwa sharti la kutotambulishwa, kimeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba kikosi cha RSF, kiliwafyatulia risasi watu hao waliokuwa katika mji wa Al-Hilaliya.
Mapigano yaongezeka jimboni la Al-Jazira nchini Sudan
Jimbo la Al-Jazira nchini Sudan limekuwa eneo kuu la mapigano kufuatia kutoka kwenye kikosi hicho cha RSF kwa kamanda mmoja Abu Aqla Kaykal.
Watu 50 wauawa katika mashambulizi ya wanamgambo wa RSF Sudan
Hivi karibuni, Kaykal alijiunga na jeshi la Sudan, pamoja na kile ambacho jeshi hilo lilieleza kuwa idadi kubwa ya wapiganaji wake, katika tukio la kwanza la kujiondoa kwa afisa wa ngazi ya juu kutoka kikosi hicho cha RSF.
RSF yaishambulia pakubwa Al-Jazira kati ya Oktoba 20 na 25
Kulingana na mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Clementine Nkweta-Salami, RSF ilianzisha mashambulizi makubwa katika maeneo ya mashariki ya jimbo la Al-Jazira kati ya Oktoba 20 na 25.Zaidi ya watu 120 wauawa katika mji wa Sariha nchini Sudan
Nkweta-Salami ameongeza kuwa wanamgambo hao walitekeleza mauaji ya watu wengi, unyanyasaji wa kingono, uporaji mkubwa wa masoko na nyumba pamoja na uteketezaji mkubwa wa mashamba.
Mzozo nchini Sudanulizuka katikati ya mwezi wa Aprili 2023 kati ya jeshi la serikali linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan, na kundi la RSF linaloongozwa na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo.