1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Watu 13 wafa maji wakijaribu kwenda barani Ulaya

29 Oktoba 2024

Raia 13 wa Misri wamekufa baada ya boti waliyokuwa wanasafiria kwenda barani Ulaya kuzama kwenye pwani ya Libya. Mtu mmoja tu ndiye aliyenusurika kwenye mkasa huo.

Watu 13 wafa maji wakijaribu kwenda barani Ulaya
Watu 13 wafa maji wakijaribu kwenda barani UlayaPicha: Jana Stallein/SOS Humanity

Kulingana na taarifa za maafisa wa Libya na kutoka kwenye shirika moja linalotoa misaada kwa wakimbizi, mtu mmoja ndiye aliyenusurika kwenye mkasa huo.

Shirika hilo la misaada la nchini Libya, Al-Abreen, limesema boti hiyo ilizama umbali wa kilomita 60 katika pwani ya mji wa Tobruk wa mashariki mwa Libya jana Jumatatu jioni.

Wahamiaji 11 wafa baharini, 60 hawajulikani waliko

Shirika hilo limesema mtu huyo aliokolewa pamoja na maiti zilizoopolewa. Idara ya kupambana na uhamiaji haramu huko Tobruk pia imethibitisha tukio hilo.

Katika miaka ya hivi karibuni, Libya limekuwa ni taifa linaloongoza kuwa ni sehemu wanayoitumia wahamiaji wanaokimbia vita na umaskini kutoka barani Afrika na katika nchi za Mashariki ya Kati wanaojaribu kwenda barani Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW