Janga
Watu 13 wafariki baada ya maporomoko ya ardhi Uganda
28 Novemba 2024Matangazo
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa maafisa wanatarajia idadi ya vifo huenda ikapanda hadi watu 30. Maporomoko hayo ya ardhi yalitokea baada ya mvua kubwa kunyesha jana usiku katika wilaya ya Bulambuli iliyoko eneo la milimani. Eneo hilo kumbukwa na maporomoko ya ardhi ya mara kwa mara.
Kiasi ya watu 30 wahofiwa kufa kwenye maporomoko ya ardhi Uganda
Gazeti la Daily Monitor limeripoti kuwa nyingi ya miili iliyopatikana mpaka sasa ni ya watoto wadogo. Picha na vidio za watu wakichimba kwenye matope kuwatafuta waathirika zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Baadhi nyumba zilifukiwa kabisa na matope. Ofisi ya waziri mkuu ilitoa tahadhari ya maafa jana ikisema kuwa mvua kubwa kote nchini humo ilikuwa imeharibu barabara nyingi.