1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 13 wameuawa katika mashambulizi ya RSF Sudan

9 Oktoba 2025

Watu 13 wameuawa katika shambulizi la RSF nchini Sudan, baada ya wanamgambo hao kuushambulia msikiti uliokuwa unatumika kuwahifadhi watu wasio na makaazi katika mji wa El-Fasher.

Sudan 2019 | Wanamgambo wa RSF
Wangambo wa RSF waliuvamia msikiti uliowahifadhi watu wasio na makaazi Picha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Mtu mmoja anayeishi karibu na eneo hilo amesema shambulizi hilo lilitokea Jumatano mchana.

Amesema baada ya shambulizi hilo, walitoa miili ya watu13 kutoka kwenye kifusi na kisha kuwazika.

Mtu mmoja aliyenusurika katika shambulizi hilo amesema kulikuwa na familia 70 ndani ya msikiti huo, baada ya RSF kuingia ndani ya nyumba zao.

Watu 20 wajeruhiwa

Amesema shambulizi hilo limewajeruhi pia watu wengine 20 na kuharibu sehemu ya msikiti huo.

Mashambulizi yanayofanywa sasa ya RSF dhidi ya El-Fasher ni mabaya zaidi tangu walipoanza kupambana na jeshi la Sudan, mnamo Aprili 2023.

Mashambulizi hayo yanafanyika ndani ya muda wa saa 24, baada ya RSF kuwaua watu 12 katika hospitali kuu ya mji wa El-Fasher ambao umezingirwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW