1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Watu 13 wameuwawa katika mapigano Pakistan

14 Mei 2023

Jeshi nchini Pakistan limesema zaidi ya watu 12 wameuawa katika mapiganop ya usiku kucha kati ya wanajeshi wa Pakistan na wanamgambo waliovamia kituo chao na kuziteka familia zao.

Pakistanischer Ex-Premier Khan vorübergehend freigelassen
Picha: W.K. Yousafzai/AP/dpa/picture alliance

Taarifa yao inasema wapiganaji waliosheheni zana za kijeshi walilivamia eneo la kijeshi la Frontier Corps huko Muslim Bagh, jimboni Balochistan na kuteka familia tatu katika jengo la makaazi. Hadi wakati huu hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, lakini makundi ya yanayopigania kujitenga kwa jimbo hilo la kusini magharibi wamekuwa mara kwa mara wakivilenga vikosi vya usalama. Vile vile kundi la Taliban la Pakistan lina nguvu kubwa katika eneo hilo. Pakistan imeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi tangu kundi la Taliban la Afghanistan kurejea madarakani mwaka 2021.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW