MigogoroUkraine
Watu 13 wauawa na wengine 113 wajeruhiwa Zaporizhzhia
9 Januari 2025Matangazo
Mamlaka imesema miili kadhaa imetapakaa barabarani huku shughuli za usafiri wa umma zikiathirika.
Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine imesema kupitia mtandao wa Telegram kwamba majengo ya ghorofa, viwanda na miundombinu mengine imeharibiwa pia katika shambulio hilo.
Gavana wa eneo hilo, Ivan Fedorov amewaambia waandishi wa habari kuwa Urusi ilitumia mabomu mawili ya kurushwa kwa ndege yanayoongozwa kuelekea kwenye shabaha, kushambulia eneo hilo la maakazi ya watu.
Kulingana na gavana huyo, watu 10 kati ya 60 waliopelekwa hospitali wako katika hali mbaya na kuongeza kuwa, Alhamisi itakuwa siku rasmi ya maombolezo.