1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 13 wauawa na wengine 57 wajeruhiwa huko Beirut

22 Oktoba 2024

Wizara ya afya ya Lebanon imesema mapema leo kuwa watu 13, akiwemo mtoto, wameuawa na wengine 57 kujeruhiwa kufuatia shambulizi la Israel karibu na hospitali ya Hariri iyopo kusini ya Beirut siku ya Jumatatu.

Lebanon Beirut | Uharibifu baada ya shambulio la anga la Israel
Vikosi vya Lebanon vinachukua hatua za usalama kuzunguka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Rafik Hariri baada ya shambulio la Israel karibu na eneo hilo, na kuua watu 4 na kujeruhi 24 huko Beirut, Oktoba 22, 2024.Picha: Houssam Shbaro/Anadolu/picture alliance

Israel imesema hospitali ya Hariri haikuwa sehemu ya shambulizi hilo bali ililenga ngome ya kundi la Hezbollah.Kwa upande wa jeshi la Israel katika taarifa yake iliyotolewa leo limesema limevishambulia vituo kadhaa vya kuhifadhia silaha vya kundi la Hezbollah na kambi za kijeshi usiku kucha ikiwemo na kambi muhimu ya jeshi la majini mjini Beirut. Huko Gaza, Takriban watu watano wameuawa baada ya shambulizi la Israel hayo ni kwa mujibu wa wahudumu wa afya. Hilali Nyekundu ya Palestina imeripoti kuwa kulikuwa na matukio ya kutisha wakati wa usafirishaji wa miili, ambayo ni pamoja na watoto. Watu wengine 27 walijeruhiwa katika shambulizi la mizinga katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia. Wizara ya afya ya Gaza imesema takriban Wapalestina 42,718 wameuawa na wengine zaidi ya laki moja wamejeruhiwa huko Gaza tangu Oktoba 7 mwaka uliopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW