1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaBrazil

Watu 143 wafariki dunia Brazil kutokana na mafuriko

13 Mei 2024

Idadi ya vifo kutokana na mvua iliyosababisha mafuriko katika jimbo la Rio Grande do Sul nchini Brazil imeongezeka na kufikia watu 143.

Athari ya mafuriko nchini Brazil
Athari ya mafuriko nchini BrazilPicha: Gustavo Basso

Mamlaka nchini Brazil imesema watu wengine 125 hawajulikani waliko katika jimbo hilo la kusini mwa Brazil ambapo viwango vya maji kwenye mito inaripotiwa kupanda. Idara ya hali ya hewa imesema mvua zinazoendelea kunyesha "zinatia wasiwasi."

Mnamo siku ya Jumamosi, serikali ilitangaza kitita cha dola bilioni 2.34 kwa matumizi ya dharura ili kushughulikia janga hilo ambalo limesababisha zaidi ya watu 538,000 kuyahama makazi yao.

Soma pia: Mafuriko yaua watu 75 na kujeruhi wengine 155 Brazil 

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amesema serikali kuu itajenga upya miundombinu yote iliyoharibiwa na mvua katika jimbo hilo la Rio Grande do Sul.

Kwa upande wake, Rais Joe Biden wa Marekani amesema utawala wake unawasiliana na Brazil kwa lengo la kutoa msaada kwa waathiriwa wa mafuriko.