1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroNiger

Watu 15 wameuwawa katika mashambulizi ya "kigaidi" Niger

15 Agosti 2024

Wengine kadhaa wamejeruhiwa katika kile kinachoitwa mashambulizi ya "kigaidi" yaliyofanywa katika vijiji magharibi mwa Niger karibu na mpaka wa Burkina Faso.

Mashambulizi ya kigaidi yanafanyika mara kwa mara katika nchi za Sahel huko Afrika Magharibi
Mashambulizi ya kigaidi yanafanyika mara kwa mara katika nchi za Sahel huko Afrika MagharibiPicha: AFP/Getty Images

Haya yamesemwa na jeshi la Niger. Jeshi hilo linasema kwamba kijiji cha Mehana ni miongoni mwa vijiji sita vilivyolengwa katika eneo la Tillaberi huko Niger, linalopakana na Mali na Burkina Faso.

Eneo hilo linadaiwa kuwa maficho ya wapiganaji wa jihadi walio na mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu na Al-Qaeda. Raia wa Mehana hulengwa na mashambulizi ya a wanajihadi hao mara kwa mara jambo linalosababisha idadi kubwa ya watu kuachwa bila makao.

Niger inaongozwa na utawala wa kijeshi uliochukua madaraka katika mapinduzi yaliyofanyika Julai mwaka jana, kutokana na kile jeshi ilichosema ni hali duni ya usalama inayozidi kuwa mbaya.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW