1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 150 wahofiwa kufariki baada ya boti kuzama ziwa Kivu

Sylvia Mwehozi
17 Aprili 2019

Kiasi ya watu 150 hawajulikani walipo na kuhofiwa kupoteza maisha katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuwepo na taarifa jana jioni za kuzama kwa feri katika ziwa Kivu mashariki mwa mchi.

Demokratische Republik Kongo Stadt Goma Kivu See Panorama Freies Format
Picha: Creative Commons/Sascha Grabow

Kiasi ya watu 150 hawajulikani walipo na kuhofiwa kupoteza maisha katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuwepo na taarifa jana jioni za kuzama kwa feri katika ziwa Kivu mashariki mwa mchi. Rais Felix Tshisekedi aliandika katika ukurasa wa Twita kuwa anasikitishwa na kuzama kwa boti kwenye ziwa Kivu na kutoa pole kwa familia. Waziri wa usafiri wa mkoa Jaqcueline Ngengele amelieleza shirika la habari la dpa, kuwa kati ya abiria wanaokadiriwa kufikia 200 ni abiria 40 tu ambao wameokolewa. Hadi sasa watu watatu ndio waliothibitishwa kupoteza maisha. Waziri huyo amesema hali mbaya ya hewa na kujaza kupita uwezo vimechangia ajali . Afisa mwingine wa mkoa amesema abiria wengi hawakuwa wamevaa majaketi ya kujiokoa. Ajali za kuzama kwa boti zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika maziwa na mito nchini Congo. Mwaka 2001 watu kati 100 hadi 150 walifariki baada ya boti kuzama katika ziwa Kivu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW