1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Watu 16 wauwawa katika mashambulizi ya roketi Darfur

22 Julai 2023

Takriban raia 16 wameuwawa baada ya roketi kuangukia nyumba katika mji wa Darfur magharibi mwa Sudan.

Sudan Kämpfe
Picha: Stringer/IMAGESLIVE via ZUMA Press Wire/picture alliance

Haya ni kwa kujibu wa chama cha wanasheria katika eneo hilo.

Tukio hilo limejiri wakati wa makabiliano kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha dharura cha RSF. Chama cha wanasheria kimesema mtu mmoja ameuwawa baada ya kupigwa risasi.

Soma pia: UN: Watu 87 walikwa katika kaburi la pamoja Darfur

Mapigano huko Darfur ambako ni ngome ya RSF, yamejikita karibu na mji wa Nyala, baada ya mapigano ya El Geneina ambapo Umoja wa Mataifa iliripoti kuwepo kwa vitendo vya ukatili.

Mapigano pia yameendelea ndani na karibu na mji wa Khartoum huku wakaazi wakiripoti mashambulizi ya kwanza ya angani kwenye vijiji vya jimbo la Al-Jazirah kaskazini, kusini mwa mji mkuu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW