1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaIran

Watu 16 wapoteza maisha ajali ya gari Iraq

2 Septemba 2023

Watu 16 wengi wakiwa ni mahujaji kutoka Iran, wamekufa usiku wa kuamkia leo kutokana na ajali ya gari iliyotokea kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad.

BdTD Irak irakische schiitische Pilger vor religiösem Fest Arbaeen
Mamilioni ya mahujaji wa Kishia hufanya safari kwenda eneo takatifu la Karbala kwa sherehe za Arbaeen.Picha: Asaad Niazi/AFP

Hayo yameripotiwa na Shirika la Habari la Iraq, INA, likinukuu duru kutoka idara za afya za jimbo kulikotokea ajali hiyo. Mkuu wa Idara ya Afya ya jimbo la Salaheddine, Khaled Burhan, amesema ajali hiyo ya kutisha imetokea baina ya wilaya za Dujail na Samarra na kwamba mbali ya vifo, watu wengine 13 wamejeruhiwa.

Hata hivyo afisa huyo hakutoa ufafanuzi zaidi juu ya chanzo cha ajali hiyo lakini amesema wengi ya waliopoteza maisha ni mahujaji wa madhehebu ya waislamu wa kishia kutoka Iran.

Kila mwaka mamilioni ya mahujaji wa Wakishia, wengi kutoka Iran, hufanya safari za hija kwenye eneo takatifu la Karbala kwa sherehe za Arbaeen, ikiwa ni moja ya mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW